TFF YAMTOA KIFUNGONI BUSWITA KWA SHARTI ZITO - Rhevan Media

TFF YAMTOA KIFUNGONI BUSWITA KWA SHARTI ZITO



Kiungo mpya wa Yanga, Pius Buswita ameruhusiwa kuichezea klabu hiyo kwa sharti la kulipa Sh10milioni alizochukua Simba ikiwa ni sehemu ya makubaliano yake ya awali.
Mwenyekiti wa kamati ya katiba sheria hadhi na wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala alisema baada ya kikao na wajumbe wa kamati hiyo jana Jumanne wamefikia makubaliano ya kumpa ruhusa ya mchezaji huyo kucheza Yanga.
Mwanjala alisema katika kikao hicho Simba iliwakilishwa na Said Tully na Yanga alikuwa Baraka Dausdedit na wakafikia makubalino ya mchezaji huyo kulipa fedha hizo alizopokea kutoka Simba ili kuanza kuitumikia Yanga.
"Kamati yangu imempa ruksa Buswita kucheza Yanga, lakini kabla ya kuanza kucheza anatakiwa kulipa Sh 10 milioni alizochukua kutoka Simba na kusaini mkataba wa awali," alisema Mwanjala.
"Baada ya kulipa fedha hizo kwa muda wowote  atapata ruksa ya kuitumikia Yanga na mwenyewe alikili kuwa kuwa kweli alisaini mkataba na atarudisha fedha za Simba," alisema.
Mjumbe wa kamati ya hiyo Robart Selasela alisema Buswita baada ya kulipa pesa ya Simba watampa onyo kali ila wachezaji wengine kuogopa kufanya jambo kama hilo.

Previous
Next Post »