- Kimbunga hicho kimeharibu nyumba na biashara, na kukatiza umeme maeneo mengi. Watu 10 wamethibitishwa kufariki kufikia sasa. Hapa ni ufukweni katika mji wa Gustavia kisiwa cha Saint-Barts
- Katika visiwa vya Virgin Islands vya Uingereza, upepo mkubwa na mawimbi vinaonekana vikisukuma meli na boti hadi ufukweni
- "Ni janga kubwa, kisiwa kimeharibiwa 95%. Nimesikitishwa sana," afisa wa kisiwa cha Saint-Martin Daniel Gibbs amesema kwenye mahojiano.
- Jeshi la Uholanzi limetoa picha za kutoka angani zikionesha uharibifu Sint Maarten, eneo la kisiwa cha St Martin linalomilikiwa na Uholanzi. Kisiwa hicho kimegawanywa mara mbili - eneo la Uholanzi na la Ufaransa.
- Katika jimbo la Puerto Rico. Nusu ya nyumba na biashara hazina umeme na maeneo mengi ya kisiwa hicho yamefurika maji.
- Ingawa Puerto Rico haijapigwa moja kwa moja, maafisa wa uokoaji wamelazimika kuondoa miti iliyoanguka pamoja na vifusi barabarani.
- Kina cha maji kinatarajiwa kupanda kwa hadi 20ft (6m) maeneo mengi ya pwani Caribbean
- Kaskazini mwa Haiti, watu waliondoa vitu vyao vya thamani kutoka kwenye paa za nyumba wakijiandaa kwa Irma.
- Kituo cha Taifa cha Vimbunga cha Marekani kimetahadharisha kwamba juhudi za kulinda maisha na mali zinafaa kuharakishwa kabla ya kimbunga hicho kupitia maeneo yanayotarajiwa kupigwa na kimbunga hicho.
- Wakazi maskini wa Santo Domingo katika Jamhuri ya Dominika wana wasiwasi kuhusu athari za upepo na maji kwenye nyumba zao.
- Richard Branson amekuwa katika kisiwa chake cha kibinafsi cha Necker, katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza wakati wa kimbunga hicho.
- Vimbunga vimekuwa vikipiga pwani ya Florida mara kwa mara lakini Irma ndicho kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kutokea Atlantiki katika kipindi cha mwongo mmoja.
- Wakazi wa Key West, Florida, wamekuwa wakijiandaa na wengine kuondoka maeneo yaliyo hatarini.
- Baadhi ya maduka Florida yameishiwa na maji ya chupa. Katika baadhi ya maeneo, kumeripotiwa makabiliano kati ya wateja wakipiganuia maji na chakula.
- Baada ya Irma, vimbunga Jose na Katia. Vinatarajiwa kufuata. Kimbunga Katia kinatishia pwani ya Mexico.
Sign up here with your email