KUTOKA UGAIBUNI : WATU 26,000 WASALIMISHA BUNDUKI - Rhevan Media

KUTOKA UGAIBUNI : WATU 26,000 WASALIMISHA BUNDUKI

A pile of guns handed in to authorities
Haki miliki ya pichaAUSTRALIAN GOVERNMENT
Image captionWatu nchini Australia wasalimisha bunduki 26,000
Watu nchini Australia wamesalismisha karibu bunduki 26,000 kwenye mpango wa kwaza wa kutoa msahama wa walio na bundukia zisizo na vibali tangu watu wengi wapigwe risasi mwaka 1996.
Msamaha huo ulianza Julai mosi kusaidia kukabiliana na ugaidi uliokuwa ukikua na kuingia kwa silaha nchini humo.
Ni haramu kumiliki bunduki isiyo na kibali nchini Australia.
Wale ambao watapatwa nje ya msamaha huo watapigwa faini ya doa 225,000 na hadi kifungo cha miaka 14 jela
Mpango huo wa sasa ambao unaendelea hadi Septemba 30, una maana kuwa watu nchini Australia wanaweza kusalimisha bunduki ambazo hazina vibali na vitu vingine kama hivvyo bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri wa sheria Michael Keenan anasema kuwa matokeo mazuri hadi sasa yataifnya nchi kuwa salama.
Polisi wanakadiria kuwa kuwa kuna hadi bunduki 260,000 haramu nchini Australia, zingine zikitumiwa kwa uhalifu na visa vya hivi majuzi vya ugaidi.
Bw. Keenan alitoa mfano wa mwanamume Haron Monis aliyetekeleza ugaidi kwenye mkahawa mmoja mjini Sydney mwaka 2014, ambaye alitumia bunduki isiyo na kibalia ambayo ilikuwa imeingizwa nchini Australia miaka 1950.
Previous
Next Post »