WAKIMBIZI WALIOKWAMA LIBYA WAPO KATIKA HALI MBAYA - Rhevan Media

WAKIMBIZI WALIOKWAMA LIBYA WAPO KATIKA HALI MBAYA

Baadhi wanasema walifikia hatua ya kuzihama nchi zao kwa ushawishi tu

Image captionBaadhi wanasema walifikia hatua ya kuzihama nchi zao kwa ushawishi tu

BBC imepata nafasi adimu ya kuingia katika kambi kubwa inayowazuia wakimbizi nchini Libya, na kukuta wakiwa katika hali mbaya.
Wanaoshikiliwa wanasema wamejazwa katika vyumba mpaka kufikia hatua ya kulala wakiwa wamesimama.
Hawana huduma muhimu kama maliwato,huku chakula kikiwa ni cha shida.

Chumba hiki kinahifadhi watu wengi kushinda uwezo wake
Image captionChumba hiki kinahifadhi watu wengi kushinda uwezo wake

Wengi wao walirubuniwa na wanaofanya biashara za kusafirisha watu na wamekwama kuingia Ulaya.
Msimamizi wa eneo hilo anasema wanahitaji misaada ya kibinaadam kuweza kuwasaidia.
Previous
Next Post »