Dar es Salaam. Mataifa matano ikiwamo Saudia Arabia, Yemen na Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAR) zimesitisha uhusiano wa kimataifa na nchi ya Qatar kwa kile kinachodaiwa taifa hilo kushirikiana na magaidi.
Nchi nyingine zilizokata uhusiano wake na Qatar ni Misri na Bahrain.
Uamuzi wa nchi hizo umetangazwa leo, Jumatatu asubuhi na taarifa kutoka Shirika la Habari la CNN zimeeleza kuwa raia wa Qatar wamepewa saa 48 kuondoka Falme za Kiarabu.
Wakati huo huo, Saudi Arabia wamesema wanafunga njia zote za uchukuzi na mawasiliano zinazoelekea Qatar ikiwamo ndege, ardhi na bandari
Sign up here with your email