MIRAJ AISHTUKIA SINGIDA UNITED - Rhevan Media

MIRAJ AISHTUKIA SINGIDA UNITED



Dar es Salaam. Nahodha wa African Lyon, Miraj Adam amegoma kujiunga na Singida United hadi pale atakapopewa mkataba rasmini.
Adam aliyemaliza mkataba wak na Lyon iliyoshuka daraka anatakiwa na Singida United kwa ajili ya mashindano ya SportPesa yanayoendela pamoja na Ligi Kuu msimu ujao.
Miraji alisema alikuwa katika mazungumzo mazuri na klabu hiyo, lakini kilichotokea walimtaka kujiunga kambini na wenzake moja kwa moja bila kusaini mkataba wowote kitu ambacho alikiona kama ni kigeni kwa upande wake.
Miraji pia alisisitiza kugoma kwake ni kutokana na klabu ya Simba nayo kuonyesha nia ya kumuhitaji huku akihofia kuonekana akiwa na jezi za Singida akiwa katika mashindano ya Sportpesa wakati akiwa hajasaini.
“Hakuna kabisa na dalili ya mkataba nimeona bora nitulie nisije nikafanya mambo ya ajabu katika maisha yangu ya soka,”alisema.
“Unajua unaweza ukaenda alafu wakataka moja kwa moja ucheze katika kombe hili sasa nachezaje wakati sina mkataba alafu vilevile kuna Simba nao wananitaka sasa nikionekana kule nacheza nitakuwa nimejialibia kabisa wakati huo huo sina mkataba,”alisema.
Klabu ya Singida United imewakosa wachezaji wengi kipindi hiki kutokana na falsafa yao ya kutaka kuwajalibisha wachezaji katika mashindano ya Sportpesa huku wachezaji hao wengi wakiwa wanahitajika na klabu nyingine.

Previous
Next Post »