Mwanza. Kocha wa timu ya soka ya shule za Mkoa wa Mwanza, Michael Otieno ametamba kuondoka na ubingwa wa mashindano ya Copa Umisseta ngazi ya Taifa yatakayoanza kesho Jumanne jijini Mwanza.
Mashindano hayo yatafanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, yatashirikisha Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Otieno alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanatwaa ubingwa kwenye soka na kwamba hakuna Mkoa unaompa wasiwasi.
Alisema kuwa vikosi vyake viwili (Wasichana na Wavulana) viko tayari kwa mapambano ila atawakosa wachezaji wawili kwenye kikosi cha wavulana.
Aliwataja watakaokosa mechi za kesho kuwa ni mshambuliaji Omary Shabani na kiungo mchezeshaji Josephat John wote majeruhi.
“Naamini wachezaji wangu hawatamuniangusha kwani amewafua vya kutosha na sasa tusubiri kujua nani tunaanza naye."
Sign up here with your email