MJUMBE SIMBA AJITOSA KUWANIA UONGOZI WA SOKA LA WANAWAKE - Rhevan Media

MJUMBE SIMBA AJITOSA KUWANIA UONGOZI WA SOKA LA WANAWAKE



Dar es Salaam. Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, Jasmin Badar Soudy amejitosa kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya chama cha soka cha Wanawake Tanzania (TWFA)  utakaofanyika Julai 8.
Akizungumza wakati wa kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo leo, Jasmin alisema kuwa amejipima na kuona anaweza kulisogeza mbele soka la wanawake nchini.
"Leo nimerudisha fomu za kuwania nafasi hii nikiamini ninaweza kusaidia maendeleo ya soka la Wanawake."
 "Muda wa kampeni ukifika, nitafafanua kwa undani kile kilichonisukuma kufanya hivi pamoja na nini nitakachokifanya kama nikipewa nafasi, " alisema Jasmin.
Previous
Next Post »