Kumeripotiwa mapigano maeneo ya mji wa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Wenyeji wanasema kuwa kundi ambalo halikutambuliwa lilifanya uvamizi mapema leo.
Msemaji wa jeshi eneo hilo aliiambia BBC kuwa mapigano yalitokea na kuongeza kuwa vikosi vyake vilizima shambulizi hilo.
Wenyeji wa Beni walisema kuwa watu waliokuwa wamejihami vikali walishambulia kambi ya jeshi na kisha wakaelekea shule na ofisi ya Meya.
- Zaidi ya wafungwa 900 watoroka gerezani DRC
- Watu 17 wafa wakihofia kuvamiwa na waasi DRC
- WHO kukabiliana na Ebola DRC
Kundi hilo kisha likachukua udhibiti wa Redio moja kwa muda wa saa moja kabla ya jishi kuitwaa tena.
Taarifa zinasema kwa watu hao walikuwa ni wa kundi la Mai Mai, na sasa utulivu umerejea baada ya makabiliano makali na jeshi.
Mai Mai ni jina llinalomaanisha, "ulinzi wangu" na kundi hilo huendesha shughuli zake ndani na nje ya mji wa Beni.
Shambulizi hilo linakuja baada ya wanamgambo kuvamia gereza moja mjini Beni wiki iliyopita ambapo watu 11 waliuawa na zaidi ya wafungwa 900 kutoroka jela.
Sign up here with your email