INDIA KUWASAFIRISHA RAIA WAKE WALIOKWAMA QATAR - Rhevan Media

INDIA KUWASAFIRISHA RAIA WAKE WALIOKWAMA QATAR

Air India plane

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIndia kuwasafirisha raia wake waliokwama Qatar
Mashirika mawili ya ndege yataanza kufanya safari zaid kuenda mji mkuu wa Qatar Doha kuwasaidia raia wa India waliokwama nchini humo kurudi nyumbani.
Shirika linalomilikiwa na serikali ya India shirika la binafsi la Jet Airways, yatafanya safari zaidi Alhamisi, kwa mujibu wa serikali.
Nchi kadha za kiarabu zikiwemo Saudi Arabia na Misri zimekata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na kuishutumu kwa kuvuruga eneo hilo.
Raia wa India ndio wahamiaji wengi zaidi nchini Qatar.
Hatua hiyo inakuja baada ya waziri wa usafri wa ndege nchini India Ashok Gajapathy Raju, kufanya mazungumzo na waziri wa mashauri ya kigeni Sushma Swaraj na kumhakikishia kuwa safari zitaongezwa kuwaruhusu raia wa India ambao hawajafanikiwa kupata tiketi kurudi nyumbani.
Taarifa ya serikali ilisema kuwa shirika la India Air, litafanya safari zaidi kati ya mji wa kusini wa Trivandrum na Doha kutoka kuania Juni 25 na terehe 8 Julai huku shirika la Jet Airways likifanya safari kati ya Mumbai-Doha-Mumbai kati ya tarehe 22 na 23 mwezi Juni.
Previous
Next Post »