Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha mapema jana kwenye ajali iliyokuwa ikihusisha safari ya kimasomo.
Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Aidha, Mh. Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge wamesakusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent kwa ajili ya kikao
Sign up here with your email