TAMBWE MAMBO MAGUMU - Rhevan Media

TAMBWE MAMBO MAGUMU



STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe juzi jumamosi  alifunga bao lake la 10 la Ligi Kuu lakini amedai kuwa msimu huu umekuwa ngumu kuliko misimu yote aliyokuwapo hapa nchini.
Tambwe ambaye ni mfungaji bora mara mbili wa Ligi Kuu, alisema; "Tangu nimeanza kucheza soka hapa nchini misimu yote ligi ikiwa dakika za mwisho mfungaji bora anakuwa amefahamika lakini msimu huu mambo yamekuwa magumu katika kuwania tuzo hiyo kwani kuna zaidi ya wachezaji watano ambao wapo vizuri."
Akizungumzia uwezekano wa kuendelea kusalia Yanga kwa msimu ujao, Tambwe alisema bado yupo kwenye majadiliko na pande mbalimbali ambapo ataamua hatma yake siku chache zijazo.
Previous
Next Post »