TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA OPEN HEART YA NCHINI AUSTRALIA YAFANYA UPASUAJI WA MOYO - Rhevan Media

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA OPEN HEART YA NCHINI AUSTRALIA YAFANYA UPASUAJI WA MOYO




UP1
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuziba matundu ya moyo kwa mgonjwa wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo. Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
UP2UP3
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu mguuni kwa mgonjwa wa moyo na kuupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba kwa jina la kitaalamu Coronary Artery Bypass Graft (CABG). Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.

Previous
Next Post »