AJALI YAJERUHI WAWILI , ZAIDI YA 60 WANUSURIKA KIFO - Rhevan Media

AJALI YAJERUHI WAWILI , ZAIDI YA 60 WANUSURIKA KIFO



Shinyanga. Watu wawili wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 60 wakinusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Ruksa Class kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Hilux katika eneo la Nhehelegani mkoani Shinyanga.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Muliro Jumanne amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo (Jumanne) saa 3.00 asubuhi wakati basi hilo likitokea jijini Mwanza kuelekea mkoani Kigoma.
Kamanda Jumanne amewataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni  Benard Bisansaba(45), ambaye ni mchumi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na Kassim Shaaban (41) ambaye ni mwandisi wa halmashauri hiyo.
“Majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu,” amesema Jumanne.


Previous
Next Post »