HABARI MBAYA HIVI PUNDE :MABASI YA ABOOD NA HAPPY NATION YAPATA AJALI NA KUJERUHI 12 MLIMA KITONGA YALIKUWA YAKITOKEA MBEYA KUELEKEA DAR - Rhevan Media

HABARI MBAYA HIVI PUNDE :MABASI YA ABOOD NA HAPPY NATION YAPATA AJALI NA KUJERUHI 12 MLIMA KITONGA YALIKUWA YAKITOKEA MBEYA KUELEKEA DAR


abood1

Wenye ndugu waliosafiri kwenye magari ya Abood na Happy Nation kutoka mbeya kwenda Dar es salaam magari hayo yamepata ajali mlima Kitonga muda huu na yamejeruhi abiria 12.                        
 Hii ni baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liliiigonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigongana na basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni , Fullshangwe imeongea na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda Kenedy Komba akiwa eneo la tukio  na ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kwamba kwa taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi  hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.PICHA KWA HISANI YA MITANDAO
abood2
Previous
Next Post »