Mawasiliano ya simu kati ya Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.
Gazeti la Washington Post liliripoti kuwa bwana Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.
Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.
Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.
Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.
Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.
Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweli
Sign up here with your email