Takriban watu 100 wamekwama katika uwanja wa ndege wa Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya kufurushwa nchini Marekani kulingana na waziri wa habari nchini humo.
Hatua hiyo inafuatia agizo la rais Donald Trump kusitisha mpango wa wakimbizi kuingia nchini humo mbali na kuzuia kuingia kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ikiwemo Yemen, Libya,Sudan na Somalia.
Waandishi wa BBC wanajaribu kuingia katika uwanja huo .
Raia hao waliwasili usiku na sasa wamekwama katika eneo la kusafiri.
Mkimbizi mmoja wa Somalia anayeishi katika kambi moja kaskazini mwa Kenya Ahmed Omar ameambia BBC kwamba amekuwa akitafuta hifadhi nchini Marekani kwa miaka 10 na sasa mipango yake imezuiliwa kutokana na agizo hilo la rais Trump.
Sign up here with your email