MKURUGENZI AMVUA MADARAKA MWALIMU MKUU WA BUNDA B KWA UDAGANYIFU - Rhevan Media

MKURUGENZI AMVUA MADARAKA MWALIMU MKUU WA BUNDA B KWA UDAGANYIFU


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa tuhuma za kushiriki kusaidia mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la nne.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kumruhusu mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia mtihani wa mwanafunzi wa darasa nne kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye hajui kusoma wala kuandika ili aweze kufaulu.

Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.

Kufuatia tukio hilo Bi. Janeth ametoa onyo kwa walimu wote wa shule zilizofanya vibaya na kuwataka kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka 2017 na kuahidi kuwavua madaraka walimu wa shule zitakazofanya vibaya.

Aidha, Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amewataka walimu wakuu, waratibu na walimu wote kutekeleza kutekeleza majukumu yao kulingana na sheria na kanun9 a utumishi wa Umma.

Mkurugenzi huyo amezizawadia shule kumi za Msingi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza Darasa la saba kwa mwaka 2016 kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu katika eneo hilo.

Utaratibu huo ulenga kutoa hamasa kwa wanafunzi na walimu wilayani humo na kuongeza juhudi katika kufundisha na kujifunza kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika Halmashauri hiyo.

Amezitaja shule zilizoingia kumi bora ni pamoja na Olympus, Daystar, St. Paul, Mzuma, Kabarimu B, Bigutu, Bukore, Kung’ombe, Kabarimu A na Bitaraguru ambazo zote zimetunukiwa vyeti vya kutambua mchango na juhudi wanazofanya.

Mayanja alisema kuwa kati ya shule hizo nne ni shule binafsi na sita za Serikali ambazo ambapo pamoja na zimekabidhiwa hundi za fedha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja


Previous
Next Post »