Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu jana ametoa pasi ya bao timu yake, AFC Eskilstuna ikipata sare ya 1-1 na Elfsborg zote za Ligi Kuu ya Sweden katika mchezo wa kirafiki nchini Hispania.
Thomas Ulimwengu
Katika mchezo huo uliofanyika mjini Barcelona, Ulimwengu aliyejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa Januari, alimsetia mshambuliaji wa Nigeria, Chidi Dauda Omeje kufunga bao hilo la AFC Eskilstuna.
Kwa wiki nzima sasa, Ulimwengu yuko Hispania na klabu yake hiyo mpya, AFC Eskilstuna kwa maandalizi ya Ligi Kuu ya Sweden, inayotarajiwa kuanza mwezi Aprili
Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Sign up here with your email