MAKONDA AUBEEP , MTANDAO WA ' WAUZA UNGA ' - Rhevan Media

MAKONDA AUBEEP , MTANDAO WA ' WAUZA UNGA '

PAUL Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameutaja mtandao wa wauzaji wa dawa za kulevya hapa jijini huku miongoni mwao, yakiwemo majina ya wasanii maarufu pamoja na wafanyabiashara mbalimbali, 
Katika mkutano wake na wanahabari hii leo jijini Dar, Makonda amesema yupo tayari kupoteza kila kitu, ikiwemo maisha yake na ukuu wa Mkoa lakini awe na majibu kwa Mungu kuhusu mchango wake katika kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na dawa za kulevya.
Wasanii Wema Sepetu, TID, Rachel, Chid Benz, Mr. Blue, Dogo Hamidu na Babuu wa Kitaa, mtangazaji wa kituo cha Clouds TV wametajwa kuwa na mahusiano na mtandao wa dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kesho asubuhi kwaajili ya mahojiano zaidi.
Christopher Fuime aliyewahi kuwa Mkuu wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi Kinondoni (RPC) ni miongoni mwa maofisa 17 wa Jeshi la Polisi waliotajwa kushirikiana kuulinda mtandao wa dawa za kulevya jijini Dar.
“Polisi wamekuwa wakiwapigia simu watuhumiwa wa uuzaji wa dawa za kulevya na kuwataarifu kuwa wanaenda kuwakamata na kisha kuwataka wawatumie fedha kwa njia ya simu. Polisi wanapoenda wanawakosa wahusika lakini wanakuwa wameshapokea fedha zao,” amesema Makonda.
Makonda amewataja watu ambao tayari wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na tuhuma za kuuza dawa za kulevya akiwemo Said Masudi Lina, Ahmed Ngahemela “Pettit Man”, Nassor Mohamed, Bakari Mohamed Khelef na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Omary.
Previous
Next Post »