KIUNGO wa zamani wa klabu ya Chelsea, New York City FC na timu ya taifa ya England, Frank Lampard (38) leo ametangaza kustaafu mchezo wa mpira wa miguu baada ya kuucheza kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 21,
Lampard ambaye mpaka anatangaza kustaafu soka ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England, mataji mawili ya Kombe la Ligi, mataji matatu ya kombe la chama cha soka nchini England (FA) na taji la Klabu Bingwa Ulaya mara moja.
Mkongwe huyo ametangaza uamuzi wake wa kustaafu soka kupitia kwenye ukurasa wake unaopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuandika waraka mrefu kwenda kwa washabiki zake na wapenzi wa soka wote ulimwenguni.
Lampard aliandika kuwa huu ndio wakati sahihi wa yeye kustaafu mpira licha ya kupokea ofa nyingi ili aendelee kucheza mpira.
“Baada ya miaka 21 ya kucheza mchezo wa soka, sasa nimeamua kwamba ni wajati muafaka wa kustaafu mpira kama mchezaji wa kulipwa.”
“Wakati huo nimepokea ofa nyingi na nzuri kutoka nyumbani na nje ya nchi ili niendelee kucheza mpira, lakini kwa umri huu wa miaka 38 najisikia sasa ni wakati wa kuanza sura mpya katika maisha yangu,” aliandika Lampard kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mpanga anatangaza kutundika daruga, Lampard amecheza jumla ya michezo 106 katika timu ya taifa, na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Chelsea baada ya kufunga mabao 211 kwa mashindano yote aliocheza.
Sign up here with your email