Rais wa Brazil Michel Temer pamoja na na viongozi wengine wa serikali wamesafiri mpaka mji wa Sao Paulo kutoa salamu za rambirambi kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva kufuatia kifo cha mke wake aliyekuwa akiugua maradhi ya kansa ya ubongo.
Lula ni miongoni mwa marais waliokubalika sana Brazil lakini kashfa ya rushwa kwenye kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobras ilimchafua.
Viongozi kadhaa wa nchi za Amerika ya Kusini wametuma salamu zao za rambirambi.
Lula na Marisa Leticia walioana miaka 43 iliyopita.
Sign up here with your email