Waendesha mashitaka nchini Ufaransa wameendeleza upelelezi kuhusiana na upendeleo wa kifedha juu ya mgombea urais nchini humo Francois Fillon juu ya malipo yaliyofanywa kwa watoto wake wawili.
Anatuhumiwa pia kufanya upendeleo wa kumlipa mkewe mara dufu wakati alipokuwa mbunge japokuwa hakuna ushahidi juu ya suala hilo.
Kwa sasa wapelelezi wanataka kujua fedha zaidi ya dola elfu 80 walizolipwa Marie na Charles Fillion wakati alipokuwa Seneta zilikuwa za nini.
Familia ya Fillion imekana kufanya jambo lolote baya.
Fillion amesema kuwa watoto wake walikuwa wakilipwa kama wanasheria kwa majukumu maalum, licha ya kwamba kwa wakati huo hakuna ambaye tiyari alikuwa mwanasheria.
Sign up here with your email