Maelfu ya watu wamekusanyika katika viunga vya Bucharest na miji mingine nchini Romania katika usiku mwingine wa maandamano baada ya serikali kupitisha sheria ya kuhalalisha baadhi ya matendo ya rushwa.
Zaidi ya watu robo milioni waliandamana siku ya Jumatano yakiwa ni maandamano makubwa tokea kuanguka kwa utawala wa kikomunisti mwaka 1989.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Sorin Grindeanu amesema kamwe hatabadilisha maamuzi hayo.
Kwa upande mwingine Rais nchi hiyo Klaus Iohannis amesema ataishauri mahakama kuhusiana na suala hilo.
Kupitia sheria hiyo, viongozi mafisadi hawatapelekwa mahakamani kama kesi zao zitahusisha ufujaji wa fedha chini ya dola elfu 48 za Marekani.
Sign up here with your email