Rais mteule wa
Marekani, Donald Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa
imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.
Katika
mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Trump aligusia majigambo
ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka
mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia
hatua ya mwisho.Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.
Bwana Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.
Sign up here with your email