Maduka
14 katika eneo la Mianzini jijini Arusha yameteketea kwa moto jana
asubuhi na kusababisha hasara mbalimbali huku jeshi la polisi
likiimarisha ulinzi na kusimamia shughuli za uokoaji wa mali
zilizosalimika.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema chanzo cha moto huo ni
hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye baadhi ya majokofu yaliyokuwa
katika baadhi ya maduka hayo.
Kamanda
Mkumbo alisema mara baada ya hitilafu hiyo, moto huo ulishika mitungi
ya gesi iliyolipuka na kuanza kusambaa kwa kasi na kuunguza maduka
hayo.
Alisema
wamefanikiwa kuokoa baadhi ya mali katika maduka tisa kati ya 14 kwa
msaada wa wananchi na wasamaria wema waliokuwa katika eneo la tukio
lakini ukubwa wa hasara bado haujajulikana.
Mmiliki
wa moja ya maduka yaliyoteketea, Zena Athuman alisema kabla ya kufungua
biashara yake, alifika katika eneo la tukio na kukuta moto huo
umeshaanza na hakufanikiwa kuokoa mali yoyote kwa kuwa moto huo ulikuwa
ukisambaa kwa kasi ya ajabu.
Shuhuda
wa tukio hilo, Julius Sangeti alisema alifika katika eneo hilo saa
11:30 asubuhi na kushuhudia moto ukiwaka katika duka kubwa la Mianzini
na kadri muda ulivyokuwa ukisonga, ndivyo ulivyokuwa ukihamia kwenye
maduka mengine na kuteketeza mali.
Sign up here with your email