Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta nane Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock kwa ajili ya kuzigawa kwa Halmashauri nne za Mkoa huo wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kusini wa Bayport Financial Services, Emmanuel Nzuttu. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Bayport Mbeya, Mohamed Kisoki akifuatiwa na wakala wake Kurwa Lighton. Picha na Mpiga Picha wetu Mbeya.
Na Mwandishi
Wetu,Mbeya
SERIKALI ya
Mkoa wa Mbeya, zimewataka watumishi wa umma katika mkoa wao,hususan kupitia
ofisi zitakazonufaika na msaada wa kompyuta nane kutoka kwenye taasisi ya
kifedha ya Bayport Financial Services, kuongeza ufanisi wa kazi kwa kupitia vitendea kazi hivyo vilivyotolewa.
Hayo
yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya, Nyasenga Enock, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, kwenye
makabidhiano ya kompyuta zilizotolewa na Bayport kwa ajili ya ofisi ya
Halmashauri ya Tunduma, Ileje, Mbeya na Rungwe, huku kila ofisi ikipokea
kompyuta mbili.
Majadiliano yakiendelea katika makabidhiano hayo ya kompyuta kutoka Bayport Financial Services mwishoni mwa wiki, mkoani Mbeya.
Akizungumzia
hilo, Enock alisema kwamba haitakuwa na maana kama msaada wa kompyuta za
Bayport hautaongeza ufanisi kazini na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa
kutumia vyema vitendea kazi hivyo vipya vinavyoweza kuleta tija kama kila
mtumishi atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuwatumikia wananchi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock akigawa kompyuta hizo kwa wahusika baada ya kukabidhiwa na Bayport Financial Services.
Sign up here with your email