GUARDIOLA : UBINGWA EPL NI NDOTO - Rhevan Media

GUARDIOLA : UBINGWA EPL NI NDOTO

Sehemu ya ulinzi ya Man City inalalamikiwa kuwa dhaifu
Image captionSehemu ya ulinzi ya Man City inalalamikiwa kuwa dhaifu
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa inaweza kuondoka katika zile timu zinazowania ubingwa baada ya kupokea kichapo cha 4-0 kutoka kwa Everton.
Kwa sasa City wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 52.
Alipoulizwa kama alama 10 ni nyingi sana alijibu ndio sio rahisi kuzifikia.
Man city hawapo imara sana wanapoingia katika eneo la 18
Image captionMan city hawapo imara sana wanapoingia katika eneo la 18
Guardiola, mwenye miaka 45, amewaambia wachezaji wake kuungana wakati huu wa kipindi kigumu na kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa msimu.
''Mwishoni mwa msimu tutajitathimini kiwango chetu,ufundishaji ulikuwaje na wachezaji walikuwaje.
Baada ya hapo tutaamua kwa pamoja.
Mwanzoni mwa msimu Pep alinukuliwa akisema kitu kigumu Uingereza ni kuendesha gari kushoto pekee
Image captionMwanzoni mwa msimu Pep alinukuliwa akisema kitu kigumu Uingereza ni kuendesha gari kushoto pekee
Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya tano.
Previous
Next Post »