ACT WAZALENDO WAVUNJA UKIMWA WAMJIBU POLEPOLE WA CCM NA KUMUUMBUA KWA KAULI HII HAPA - Rhevan Media

ACT WAZALENDO WAVUNJA UKIMWA WAMJIBU POLEPOLE WA CCM NA KUMUUMBUA KWA KAULI HII HAPA

Tokeo la picha la ACT WAZALENDO
Chama cha ACT-Wazalendo, kimemjibu Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole kwa kumueleza kuwa kazi chama cha siasa ni kuhangaika na matatizo ya wananchi.

Juzi, Polepole aliwataka wapinzania kuacha  kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha kisiasa huku akitolea sakata la njaa na tetemeko la ardhi liliotokea Bukoba.

Akizungumza na wanahabari jana (Jumatano) katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma kwa chama hicho, Ado Shaibu amesema  kukabiliana na matatizo ya wananchi  ndiyo mtaji sahihi wa kisiasa.

"Chama cha siasa lazima kishughulike na matatizo ya wananchi, kisichojishughulisha na matatizo ya wananchi kitakufa,"amesema Shaibu.
Previous
Next Post »