URUSI NA UTURUKI WAFANYA MASHAMBULIZI YA PAMOJA SYRIA - Rhevan Media

URUSI NA UTURUKI WAFANYA MASHAMBULIZI YA PAMOJA SYRIA

Urusi ina ndege katika kituo cha Hmeimim kilicho nchini SyriaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUrusi ina ndege katika kituo cha Hmeimim kilicho nchini Syria
Urusi na Uturuki zimefanya mashambulizi yao ya kwanza ya pamoja, dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Syria.
Islamic State ililengwa katika vitongoji vya mji wa al-Bab mkoani Aleppo, ambapo Uturuki ilikumbwa na maafa makubwa mwezi uliopita ikipigana na Islamic State.
Msemaji wa Urusi Luteni Sergei Rudskoi amesema kuwa mashambulizi hayo ya pamoja yamekuwa yenye mafanikio makubwa.
Urusi na Uturuki wamengilia pakubwa vita vya Syria.
Mji wa al-Bab ulio umbali wa kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki, umekuwa ukilengwa na harakati za Uturuki zenye lengo la kuwatimua wanamgambo wa Islamic State na vikosi vya Kurdi.
Ndege za Marekani nazo ziliendesha mashambulizi mapema wiki hii pia kwa ushirikiano na Uturuki.
Ndege za Uturuki za F-16 zilishirikiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNdege za Uturuki za F-16 zilishiriki

Previous
Next Post »