Vijana wanaotoka katika halmashauri za
wilaya ya Kahama Mji,Ushetu,Msalala na Manispaa ya Shinyanga wamekutana
katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo
la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative
(AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI.
Bonanza hilo la michezo limejumuisha
vijana 150 wenye umri kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za
vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na shirika la AGPAHI kwa kushirikiana
na halmashauri za wilaya husika.
Akifungua bonanza hilo katika uwanja wa
taifa mjini Kahama leo Jumamosi Desemba 17,2016,mgeni rasmi Dr. Anthony
Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama,alisema bonanza hilo ni kwa
ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha
vipaji na kujifunza.
“Vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 12
vilivyopo katika halmashauri nne za mkoa wa shinyanga,ambazo ni
Msalala,Kahama mji,Ushetu na manispaa ya Shinyanga”, alisema Kasomelo.
Dr.
Kasomelo alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa kuendelea
kuwa karibu na vijana huku akiwaasa vijana hao kuendelea kuwa wafuasi
wazuri wa huduma za afya ili kuboresha afya zao ili waweze kutimiza
ndoto zao.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wa
halmashauri za wilaya kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la AGPAHI
hasa katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika huduma za
afya hususani kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane
katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi.
Awali akizungumza katika bonanza hilo,
Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane
Kashumba alisema wafadhili wa bonanza hilo ni shirika la Uingereza
linalofadhili huduma za kuboresha maisha ya watoto (Children’s
Investment Fund Foundation -CIFF).
Kashumba alibainisha kuwa shirika la
AGPAHI limeanzisha klabu 12 za vijana zenye wastani wa vijana 20 – 70
walio katika rika balehe.
“Lengo la
vikundi hivi ni kuwakutanisha vijana kila mwezi ili waweze kujifunza
pamoja masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya msukumo rika kwa
vijana,kushirikiana katika kutatua changamoto zao na njia za kujikinga
na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi vijana hao wameendelea
kunufaika na elimu hiyo”,alieleza Kashumba.
Miongoni
mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta
Kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba nyimbo na kucheza muziki
ambapo washindi waliibuka na zawadi mbalimbali.
Bonanza hilo limehudhuriwa na wadhibiti
wa Ukimwi kutoka halmashauri za wilaya,wasimamizi wa klabu za
vijana,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na wadau mbalimbali wa michezo
na mambo ya afya.
Angalia matukio katika picha yaliyojiri uwanjani hapa chini
Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la
AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba akizungumza wakati Bonanza la
michezo katika uwanja wa taifa wa mjini Kahama
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka
hospitali ya mji wa Kahama akifungua bonanza hilo la vijana
lililokutanisha vijana 150 ambapo mbali na kulipongeza shirika la AGPAHI
alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao kupenda shule
Katikati ni mgeni rasmi Dr. Anthony
Kasomelo akizungumza wakati wa kufungua bonanza la michezo.Kushoto ni
Mhudumu wa jamii pia Afisa tabibu kutoka kituo cha afya cha Kolandoto
katika manispaa ya Shinyanga Maryciana Bruno ,aliyeinama kulia ni Mganga
mfawidhi zahanati ya Segese Denis Ngatale
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akiteta jambo na Jane Kashumba
Timu ya mpira wa miguu kutoka
halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuanza mchezo baina yao
na timu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wakipiga picha kabla ya mchezo
Wachezaji wa timu ya halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI
Dawati la ufundi timu ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala.
Mchezo kati ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala ukiendelea
Mchezo unaendelea ambapo hadi kipenga
cha mwisho kinapulizwa Kahama mji walikuwa wanaongoza kwa kuibamiza timu
ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Mbio za magunia ukiendelea kati ya
vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(waliovaa nguo za bluu) na
wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikiendelea
Mbio za magunia zikiendelea ambapo hadi
mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Esther Peter kutoka Ushetu
(aliyevaa nguo nyeupe),wa pili Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya
Shinyanga(wa kwanza kulia)
Mbio za magunia upande wa vijana wa
kiume kutoka manispaa ya Shinyanga (waliovaa nguo za bluu) na wasichana
kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikachukua nafasi
Mchezo unaendelea,ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Ali Seleman,wa pili Isack Kiwila
Mchezo wa kufukuza kuku upande wa vijana wa kike ukiendelea
Vijana wakiendelea kukimbiza kuku
Helena Daudi kutoka manispaa ya
Shinyanga akiwa amebeba kuku baada ya kufanikiwa kumkamata na kisha
kuondoka naye kama zawadi ya ushindi
Vijana wa kiume nao walifukuza kuku
Kijana Peter Kulwa naye akaondoka na kuku baada ya kufanikiwa kumkamata
Mchezo wa kuvuta kamba nao
ulikuwepo,picha ni kushoto ni vijana wa kike kutoka Kahama mji,Ushetu na
Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba na vijana wa kike kutoka
manispaa ya Shinyanga(kulia).Waliopo katikati ni Dr. Anthony Kasomelo
kutoka hospitali ya mji wa Kahama na Afisa mradi wa watoto kutoka
Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba wakitoa maelekezo kwa
vijana hao kabla ya mchezo huo wa kuvuta kamba
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuvuta kamba
Katika mchezo huo wa kuvuta kamba vijana kutokaUshetu,Msalala na Kahama Mji waliibuka washindi
Vijana wa kiume kutoka Kahama Mji,Ushetu
na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba dhidi ya vijana kutoka
manispaa ya Shinyanga
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakikazana kuvuta kamba ingawa hata hivyo walishindwa katika mchezo huo
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakiimba shairi
Walezi wa vijana na vijana wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Vijana kutoka Kahama mji wakiimba
Kulia ni Dr. Selemani Wambili kutoka
Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na mlezi wa vijana kituo cha Segese
katika halmashauri ya Msalala wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Vijana wakiwa eneo la tukio
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakicheza muziki
Vijana wakionesha kipaji cha kucheza
Kijana akiimba wimbo
Vijana wakishindana kucheza muziki
Wajumbe wa kamati ya kutoa zawadi kwa
washindi katika michezo iliyofanyika uwanjani wakijadili jambo kabla ya
kuanza kugawa zawadi kwa washindi.Aliyekaa kushoto ni Dr. Selemani
Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa,kulia kwake ni mhudumu wa jamii
kutoka kituo cha Kolandoto Maryciana Bruno.Waliosimama wa kwanza ni
kushoto ni mlezi wa watoto kituo cha Kambarage Glory Assey akifuatiwa na
mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora
Selutongwe.Kulia ni mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomela akijiaandaa kupokea
majina ya washindi ili awape zawadi
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akitoa
zawadi ya kombe kwa Timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala walioibuka
washindi baada ya kuifunga timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Vijana wakifurahia baada ya kupewa zawadi ya kombe
Vijana waliofunga magoli manne na kuipa ushindi timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala wakipokea zawadi ya saa kila mmoja
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakipokea zawadi kombe kwa kuibuka wachezaji bora wa muziki
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo
akimkabidhi zawadi ya saa Esther Peter kutoka Ushetu aliyekuwa mshindi
wa kwanza katika shindano la mbio za magunia
Mshindi wa pili mbio za magunia upande wa vijana wa kike Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa kwanza mbio za magunia upande wa vijana wa kiume Ali Seleman kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa pili mbio za magunia Isack
Kiwila kutoka manispaa ya Shinyanga akishikana mkono na mgeni rasmi
kabla ya kupokea zawadi ya saa
Kijana aliyeonesha kipaji cha kucheza muziki akipokea zawadi ya begi
Mlezi wa vijana katika kituo cha
hospitali ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth Lubasha akijiandaa kupokea
vifaa vya shule ikiwepo soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea
Mlezi wa vijana katika kituo cha Segese Kanzaga Fabian akipokea vifaa vya shule kwa ajili ya vijana wake
Mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya
Kahama mji Flora Selutongwe akiwa amebeba zawadi ya soksi na kalamu kwa
ajili ya vijana anaowalea
Sign up here with your email