Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemteua Bi. Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa
Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
Uteuzi huo umefanywa leo (Desemba
17, 2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili
uliohusisha waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
Vilevile Kamati ya Utendaji
imefanya mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati
Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili Richard Sinamtwa.
Wajumbe wengine walioongezwa
kwenye Kamati hiyo ni Bw. Adam Mihayo na Bw. Hassan Hassanoo ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
Wakili Raymond Wawa ameteuliwa
kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Bw.
Joseph Mapunda ambaye ameomba kupumzika.
Pia Bibi Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.
Sign up here with your email