Meya mteule wa manispaa ya
Kigamboni mhe. Maabadi Sulemani Hoja aliye simama akitoa neno la
shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa Meya.
Na John Luhende
mwambawahabari
Uchaguzi wa Meta na Naibu Meya wa manispaa ya Kigamboni
umefanyika kwa amani na utulivu ambapo wagombea wa chama cha Mapinduzi
CCM wameibuka na ushindi wa nafasi zote mbili.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi
huo mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni katibu Tawala wa Wilaya ya
Kigamboni Rahel Muhando amemtangaza Diwani wa kata ya Pembamnazi
Mhe. Maabadi Suleiman Hoja (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Meya
baada ya kupata kura 9 na kumshinda Mgombea Celestine Maufi wa CHADEMA
aliye pata kura 5 kati ya kura zote 15 ambapo Kura moja iliharibika.
Kwa upande wa nafasi ya Naibu meya
Mhe. Amin Mzuri Sambo Diwani wa kata Kibada ameshinda nafasi hiyo
baada ya kupata kura 10 na kumbwaga mpinzani wake Mhe. Ernest Mafimbo
(CUF) aliyepata kura 5 katiya kura zote 15 zilizopigwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Meya mteule Maabadi
Selemani hoja amewashukuru wapigakura wote walioshiriki uchaguzi huo na
ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano bila ubaguzi wa vyama ili kuleta
Maendeleo kwa wananchi wa Kigamboni.
Naye aliye kuwa mgombea wa nafasi
ya Naibu Meya kwa upande wa UKAWA akiwakilisha Chama Cha wananchi CUF,
Ernest Ndamo Mafimbo , ameuelezea uchaguzi huo kuwa. Ulikuwa huru na
haki nakukubali kushindwa nakuahidi kushirikiana na washindi hao ili
kuwa tumikia wananchi.
“Tumekubali wenzetu wameshinda
maana hata idadi yetu sisi ilikuwa ndogo wao wlikuwa 10 na sisi
tulikuwa 5 tu kwa hiyo unaweza kuona jinsi mambo yalivyokuwa ”
Mbunge wa Kigamboni Dr Faustine
Ndungulile , akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa
uchaguzi amesema nimuda Sasa wakufanyakazi kwa kuwa mambo mengi
yalisimama kwa muda mrefu kwa kukosa baraza la madiwani kwa kwaajili
kupitisha mipango na miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Sign up here with your email