UTAFITI : KILIO CHA WATANZANI BADO NI BUNGE LIVE - Rhevan Media

UTAFITI : KILIO CHA WATANZANI BADO NI BUNGE LIVE

Utafiti wa taasisi ya Twaweza, unaonyesha asilimia 65 ya wananchi wanapenda vyombo vya habari vitoe taarifa za mambo maovu yanayofanywa na watumishi wa serikali vikiwemo vitendo vya rushwa.
bungelive_1
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Alhamisi hii, Mtendaji Mkuu wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa wananchi wengi wanataka uhuru wa kupata bunge la moja kwa moja, huku akisema asimilia 75 walisema vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri ya kufichua maovu na rushwa huku asilimia 18 wakisema havifanyi kazi nzuri.
“Kwa upande wa uhuru wa kutangaza habari, asilimia 53 wanasema vyombo vya habari viwe huru kutangaza habari yoyote huku asilimia 44 wakisema Serikali iwe na mamlaka ya kufungia magazeti,” alisema Eyakuze.
“Asilimia 65 wanasema vyombo vya habari havijawahi au kama vimewahi, ni mara chache vimekuwa vikitumia vibaya uhuru wake kwa kutangaza vitu ambavyo si vya kweli,” aliongeza.
Aidha alisema wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa ambako asilimia 95 ya wananchi waliohojiwa walisema wanapenda wananchi wawe huru kuikosoa serikali inapokosea.
Previous
Next Post »