RAIS MAGUFULI AKUBALI OMBI LA KUSTAAFU LA MKUU WA JESGI LA MAGEREZA - Rhevan Media

RAIS MAGUFULI AKUBALI OMBI LA KUSTAAFU LA MKUU WA JESGI LA MAGEREZA

Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali na kuridhia ombi la kusitisha mkataba na kustaafu kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John Casmir Minja kuanzia leo tarehe 02 Desemba, 2016.
Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Casmir Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dkt. Juma A. Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam aliyoitoa leo 2 Desemba, 2016 kwa vyombo vya Habari.
Previous
Next Post »