MGOMBEA TUCTA AFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUOMBA UCHAGUZI URUDIWE - Rhevan Media

MGOMBEA TUCTA AFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUOMBA UCHAGUZI URUDIWE

mussa-james-mnyeti
Mgombea wa nafasi ya mweka hazina katika uchaguzi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUTA) uliofanyika Novemba, 24, Mussa Mnyeti amefungua kesi Mahakama Kuu divisheni ya kazi kuomba mkutano mkuu wa uchaguzi ubatilishwe na uchaguzi urudiwe tena.
Mnyeti amesema sababu ya kufungua kesi ni mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi ambayo yalikuwa ni kinyume na katiba ya shirikisho hilo na hivyo mahakama ni sehemu sahihi ambayo inaweza kutoa maamuzi sahihi kuhusu mapungufu yaliyotokea katika uchaguzi huo.
8bf72a76-9f0a-4d5b-be8a-23ad1412a427
Share:
Previous
Next Post »