Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania
Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara
ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008. Kinapenda
kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa
Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.
Mkutano
huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara
ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo
la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa
na Benki ya NMB na wadhamini wengine unatarajia kuanza majira ya saa
mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa siku mbili mfululizo.
Katika
mkutano huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya
jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa
kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa
waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu
tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine.
Aidha
katika mkusanyiko huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata
muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa
kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana Blogu.
Mkutano
huu ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala
ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii
kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la
kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.
TBN inaendelea kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka
ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi
kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii
kukamilisha mchakato wa usajili wake.
Lakini
kwa namna ya pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF,
NHIF, SBL, na Coca Cola kwa kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili
la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli
wanazozifanya.
Kimsingi
lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya
habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna
kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi
mabaya ya mitandao hii.
TBN
inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho
wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii
katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa
mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu
ya masuala anuai ya kijamii.
Sign up here with your email