NAIBU Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema
Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi
wake na si vinginevyo.
Pia amesema
Serikali ya awamu ya Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba katika kutenda
yaliyomema kwa maendeleo ya nchi kwa kuogopa maneno ya watu ya
kuwakatisha tamaa.
Akizungumza Dar es
Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu na Kuabudu na
kuliombea Taifa la Kanisa la Tanzania Assemblies of God lililopo katika eneo la Kinzugi
Salasala, alisema Serikali itaendelea kusimamia misingi yake bila kuogopa
maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa kwani Sheria na Katiba za nchi zinatokana
na maneno yaliyopo katika vitabu vya Mungu.
Alisema watumishi
wa Mungu wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda kazi zao kwani uongozi
waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa nguvu za mtu yeyote.
" Uongozi
unatokana na Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa Waziri nilimaliza
siku mbili sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri kipindi hicho
nilikuwa shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa ,nikasema ni uweza wa
Mungu,"alisema na kuongeza kuwa
"Utawala wa
awamu ya tano tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba muendelee kutuombea
tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali katika
kutekeleza majukumu yetu,"alisema Mpina
Aidha aliziomba
familia za wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani
bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii.
"Familia za
Kikristo lazima ziwe mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira, hizi
faini tunazowapiga watu kutokana na ukiukwaji wa sheria za mazingira kwa
uchafuzi wa Mazingira, sio kama
tunawaonea bali kuwakumbusha wajibu wao "alisema
Kwa Upande
wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni alisema
watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya awamu ya tano na
viongozi wake.
Alisema roho za
uadui zilizopo na watu kusema vibaya na kuwakatisha tamaa kusiwavunje mioyo kwa
kusikiliza maneno ya watu katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa ya
taifahili na watu wake.
"Makanisa na
Misikiti tupo pamoja nanyi katika kuwaombea na kama serikali hii ikiendelea
hivi ndani ya miaka mitatu nchi yetu itabadilika,"alisema Mch.Sabuni.
Ibada maalum ya
Kuliombea Taifa, kusifu pamoja na kuimba, ilienda sambamba na uzinduzi wa Ablum
ya nyimbo za injili za mwimbaji Alfonsina Samweli pamoja na mnadawa kuuza DVDs
zenye nyimbo za injili.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa
Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji Alfonsina Samweli wa kanisa la Assemblies of God la
Kinziga Salasala Jijini Dar es Salaam akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kabrasha lenye
DVDs zenye nyimbo za Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira
Mhe. Luhaga Mpina akikata Utepe katika CD kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya
Nyimbo za Injili za mwimbaji Alfonsina Samweli.
Sehemu ya waumini wa kanisa la Assemblies of God la Salasala wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Hayupo
Pichani wakati wa ibada maalumu ya kuiombea Taifa iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam.
Sign up here with your email