Mchezaji
wa Mbao U-20, Ismail Mrisho Halfan akifanyiwa huduma ya kwanza ndani
ya uwanja mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili.
Mshambuliaji
wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi
nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba
wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi
ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.
Ismail Khalfan amefariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Government ya mjini Bukoba.
Ismail
Khalfan kabla ya kufikwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la
kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange
kumalizika kwa 2-0.
Kabla
ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa
peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na
kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika
Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima
moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Mchezaji Ismail
Mrisho Halfan wa timu ya Mbao U-20 akitolewa uwanjani na watu wa
msalaba Mwekundu baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wao
uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Mchezajiwa
Mbao U- 20, Ismail Mrisho Halfan akipandishwa kwenye gari la Zimamoto
baada ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa kwenye uwanja Kaitaba mjini
Bukoba
Gari
la zimamoto klikiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail
kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera. (Picha na Faustine Ruta)
Sign up here with your email