WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo kufanya
uchunguzi na kumpelekea taarifa ya watendaji waliohusika katika ubadhirifu wa
fedha za ujenzi wa mradi wa hospitali ya wilaya ya Monduli uliogharimu sh.
bilioni 2.7.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumapili, Desemba 4, 2016) wakati akizindua hospitali ya wilaya
ya Monduli ambayo katika ujenzi wake kulitakiwa kuwe na jengo la maabara ambalo
halipo na fedha zimeisha.
"Mkuu
wa Mkoa shirikiana na Sekretarieti yako kufanya uchunguzi na atakayebainika
kuhusika kwenye ubadhirifu huu achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu ujenzi
huu ulihusisha na jengo la maabara lakini tayari mradi umekamilika na hakuna
jengo la maabara," amesema.
Naye
Mkuu wa mkoa huo Bw. Gambo amesema tayari wameanza kufanya uchunguzi wa ujenzi
wa mradi huo baada ya kubaini kuwa umetumia kiasi cha fedha kilichotumika
hakilingani na thamani ya mradi huo.
Mkuu
huyo wa Mkoa ameahidi kufuatilia suala hilo na uchunguzi utakapokamilika
taarifa hiyo itapelekwa kwa Waziri Mkuu.
Awali,
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Zaveri Benela akisoma taarifa ya hospitali hiyo
inakabiliwa na changamoto ya jengo la upasuaji karibu na wodi ya wazazi hali
inayowalazimu kuwasafirisha wagonjwa umbali wa zaidi ya mita 300 hadi kwenye
jengo la upasuaji lililopo katika majengo ya zamani.
Pia
kukosekana kwa jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara kwenye majengo hayo
mapya hali inayochangia huduma kutolewa kwenye maeneo miwili tofauti kwa wakati
mmoja yaani katika wodi mpya na majengo ya zamani na hali hivyo inaleta
usumbufu kwa wagonjwa.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya
Monduli, Bw. Idd Kimanta kumaliza tatizo la mgogoro wa ardhi katika
kijiji cha Emairete kilichopo Monduli juu mkoni hapa baada ya kudumu kwa
miaka 20.
Mgogoro
huo ni wa shamba kubwa ambalo awali lilikuwa linamilikiwa na kampuni ya bia ya
Breweries na kisha kurejeshwa kwa kijiji hicho ambapo viongozi wa
viongozi wa zamani wa Kijiji hicho walijimilikisha kinyemela.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kusimamishwa na wanakijiji hao waliokuwa
wamebeba mabango ya kumuomba msaada wa kutatuliwa kwa mgogoro huo wakati
anatoka kudhuru kaburi la Waziri Mkuu wa zamani Hayati Moringe Sokoine.
Waziri
Mkuu alimtaka mkuu huyo wa wilaya kueleza sababu za kwa ya nini uongozi wa
wilaya umeshindwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye alifika kijijini hapo na kutoa
maelekezo.
Baada
ya maelekezo hayo Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani ya
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. John
Magufuli ambayo ipo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hasa wanyonge.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa miaka 20 na
kwamba Waziri Lukuvi alitoa maelekezo ambayo halmshauri inayafanyia kazi na
imeshindwa kuleta majibu kwa wananchi hao kutokana na ziara ya Waziri Mkuu
ambaye aliwataka watekeleze majukumu yao na wasitumie ziara yake kama
kisingizio.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali na Watanzania wote wanatambua
na kuiheshimu kazi nzuri iliyofanywa na hayati Sokoine kwa Taifa kipindi cha
uhai wake na itaendelea kuienzi. Pia Serikali itaendelea kushirikiana na
familia katika mambo mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI,
DESEMBA 4, 2016.
Sign up here with your email