Jeshi la Polisi nchini
Tanzania limewapiga marufuku wamiliki wa nyumba za starehe kuendekeza
tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi na kuwataka wazingatie
uhalali wa matumizi ya kumbi zao na uwezo wa kumbi hizo katika kipindi
cha sikukuu.
ACP Advera Bulimba
Taarifa hiyo imesema kuwa ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya ya watu.
Aidha jeshi hilo limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa kupitia kwa makamanda wa polisi wa miko pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu.
Pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka upotevu wa watoto, ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.
Sign up here with your email