Shirikisho
la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limefanya semina ya
utendaji kwa makatibu wake wote wa matawi katika mkoa wa Dar es Salaam,
kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao ili kuliimarisha
Shirikisho na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alisema, katika semina hiyo iliyofanyia Novemba 30, mwaka huu, jumla ya Makatibu 32 walihudhuria na kuondoka wakiwa wameongeza upeo wao katika kazi zao za chama.
Alisema, moja ya mambo ambayo walifundwa Makatibu hao ni namna nzuri ya kuwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata wanachama wapya miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu, kwa kuwa tegemeo na uhai wa Shirikisho hilo ni wanafunzi wa aina hiyo.
"Unajua Shirikisho linatilia mkazo sana katika kuhakikisha Makatibu wa Matawi wanashughulika kwa juhudi kubwa kuhakikisha kila wakati tunapata wanachama wapya hasa hawa wanaokuwa wanajiunga katika vyuo katika mwaka wa kwanza kwa kuwa hawa wanakuwa bado wabichi na wenye nguvu kutumikia Shirikisho na Chama kwa jumla", alisema Zenda na kuongeza.
"Shirikisho linalipa kipaumbele suala la kuingiza wanachama kutoka wale wa mwaka wa kwanza kwa sababu kuingia kwa wanavyuo wapya vyuoni kuna kuwa na maana pia kuwa wapo wanaondoka kutokana na kuhitimu masomo yao, ambao baada ya kuhitimu wanaweze kushindwa kuendelea kuwa wanachama wazuri wa shirikisho kutokana na kubanwa na shughuli nyingine".
Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akiongoza semina hiyo
🔺Washiriki
wakiwa kwenye semina hiyo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya
Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam.
Sign up here with your email