JAFFO AWAONYA WAKUU WA IDARA KUTOWANYANYASA WATUMISHI WALIO CHINI YAO - Rhevan Media

JAFFO AWAONYA WAKUU WA IDARA KUTOWANYANYASA WATUMISHI WALIO CHINI YAO



Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali  za mitaa  (TAMISEMI) Mh Suleiman Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini  katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta mabadiliko  ya  kimaendeleo katika Taifa.

Mh Jaffo ameyasema hayo  leo wakati akizungumza na watumishi wa umma  wa manispaa ya Ilala na jiji la Dar es slaam,  watendaji ,wabunge pamoja na madiwani  na kuwaelekeza wakuu wa idara kufanya kazi na kuwapa ushirikiano watumishi wa ngazi  za chini  katika idara zao na kuacha kuwanyanyasa .

‘’Nawaagiza wakuu wa idara  muache kuwa nyanyasa watumishi walio  chini yenu kwakuwa  wengi wanafanya kazi kwa hofu ya kuogopa kutumbuliwa  nakupelekea kutokuwa na amani katika maeneo yao ya kazi.’’ Alisema  Jaffo.

Aidha amesema  wizara yake itatoa ushirikiano kwa  watumishi wote wanaotekeleza majukumu yao kwa moyo na bidii na amewaagiza wakuu wa idara kuwa na utaratibu wa kutambua kazi za watumishi wanao jituma na kuvuka malengo ya kazi walio wekewa  hatakama hakuna pesa za kuwapa  angalau waandikiwe barua ama kupewa vyeti vya kutambua michango yao mahala pakazi.

Hata hivyo amempongeza  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , mkurugenzi wa jiji pamoja na madiwani  kwa kusimamia  suala  la usafi wa jiji kuwa nzuri  kwakuwa kipindi cha nyuma jiji lilikuwa halitamaniki.‘’Zamani jiji la Dar es salaam  lilikuwa chafu  lakini kwa sasa  hali imekuwa nzuri ukilinganisha na kabla ya kampeni ya usafi haijaanza.hayo amesema Jaffo.


Pamoja na hayo mh Jaffo ameuagiza uongozi  wa manispaa ya ilala kwa kushirikiana na katibu tawala  mkoa wa  Dar es salaam  kupitia upya mkataba alio pewa mpangaji katika eneo lilotolewa na Dawasco kwa ajili ya kujenga shule ya kata ya secondary  Buguruni   kutembelea eneo hilo na kisha kufanya maamuzi ili eneo hilo liweze kujengwa shule.

Previous
Next Post »