LOWASSA : CASTRO ALAMA YA MAPAMABANO - Rhevan Media

LOWASSA : CASTRO ALAMA YA MAPAMABANO

Tokeo la picha la LOWASSA
Edward Lowassa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro katika ubalozi nchi hiyo jijini Dar es Salaam.

FIEDEL Castro, mwasisi na mwanamapinduzi wa taifa la Cuba aliyefariki dunia mwishoni mwa Novemba mwaka huu, ametajwa kuwa ni ‘alama ya mapambano dhidi ya ubeberu na udikteta’,
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ametoa kauli hiyo baada ya kutia saini katika kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Cuba jijini Dar es Salaam.
Mwanasiasa huyo, alikwenda kutia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu cha rais huyo wa Cuba ikiwa ni sehemu ya kushiriki maombolezo ya kifo cha kiongozi huyo maarufu duniani. Alipokewa na mwenyeji wake balozi wa Cuba, Jorge Lopez Tormo.
“Mchango wa Castro kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ni wa aina yake,” amesema Lowassa.
Juzi Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema alienda kutia saini kitabu cha maombolezo ya kiongozi huyo.
Castro alifariki dunia Jumamosi tarehe 26 Novemba mwaka huu ambapo anatarajiwa kuzikwa kesho.
Previous
Next Post »