HUSSEIN PAMBAKALI APANDISHWA MAHAKAMANI KWA DENI LA MILIONI 75 - Rhevan Media

HUSSEIN PAMBAKALI APANDISHWA MAHAKAMANI KWA DENI LA MILIONI 75




MMILIKI wa maduka ya nguo Jijini Dar es Salaam, Hussein Mkangala (38) maarufu 'Hussein Pamba Kali' amefunguliwa mashtaka ya kesi ya madai baada ya  kushindwa kulipa Sh.Milioni 75 alizokopa kutoka kwa Anna Kiabi.
Shauri hilo lilitajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo upande wa mdai ulikuwa unasimamiwa na Wakili Jonas Nkya, wakati ule wa mdaiwa ukiongozwa na Ernest Swai.
Mbele ya Hakimu Is -Haq Kuppa, Upande wa mdai ulisema kwamba Novemba 20 mwaka jana mfanyabiashara huyo alikopeshwa kiasi cha sh. Miloni 80 kwa makubaliano atamlipa kwa kipindi walichokubaliana kitu ambacho amevunja makubaliano.
Wakili Nkya alidai Mei 22 mwaka huu mdaiwa Husseni alimtuma mdogo wake aitwaye Hassan Mkangala, apeleke fedha kiasi cha sh. Milioni 5 kwa Anna na kiasi kilichobakia hakulipa tena.
Kwa upande wa utetezi wao waliomba mahakama hiyo iwape muda wa siku 6 ili waweze kujibu madai hayo. Hivyo Hakimu Kuppa aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena. Lakini Mdaiwa hakuwepo mahakamani.



Previous
Next Post »