MIKOA ya Mtwara na Geita imethibitisha kutoshiriki mashindano ya
taifa ya netiboli yatakayofanyika Dodoma kuanzia Desemba 29 hadi Julai 7
mwakani, imeelezwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Annie Kibira alisema jijini Dar es Salaam kuwa, mikoa hiyo imetoa sababu tofauti za kutoshiriki mashindano hayo.
Alisema mkoa wa Geita umesema hadi sasa mambo yao hayajakaa sawa wakati ule wa Mtwara ambao umeshindwa kushiriki kwa miaka mingi, wenyewe ulisema “mambo sio mazuri.”
Alisema Chaneta imepeleka barua kwa makatibu tawala wa mikoa yote na wanatarajia kuanza kupata barua za uthibitisho kabla ya Desemba 10, ambao ndio mwisho wa kuthibitisha.
Kibira alisema kuwa ni muhimu sana kwa timu zikathibitisha kushiriki mapema kwani hiyo itaiwezesha Chaneta kupanga bajeti vizuri kwani timu shiriki zinagharamiwa chakula na malazi wakati wote wa mashindano.
Kibira aliziomba timu za mikoa kujiandaa vizuri kwa mashindano hayo ili kuleta upinzani bala ya kushiriki kwa mazoea kila mwaka.
“Vyama vya mikoa vijitahidi kuziandaa vizuri timu zao ili viweze kutoa ushindani na kuyafanya mashindano kuchamka badala ya kushiriki kimazoa tu, “alisema Kibira.

Sign up here with your email