ARDHI YA WAWEKEZAJI KUKAGULIWA NCHI NZIMA - Rhevan Media

ARDHI YA WAWEKEZAJI KUKAGULIWA NCHI NZIMA

Tokeo la picha la WAZIRI WA ARHI NA MAKAZISERIKALI imetangaza kuanza mchakato wa ukaguzi wa mashamba na maeneo makubwa ya ardhi waliyopewa wawekezaji ili kujiridhisha na mikataba waliyoingia ili kuona kama yanatumika na kwamba serikali imetangaza kuwanyang’anya watakaobainika kutoyatumia kwa shughuli zilizokusudiwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza katika majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma alisema tayari maelekezo yameshatolewa kwa wakuu wa mikoa kufanya ukaguzi kwa wote waliopewa mashamba makubwa na maeneo makubwa ya ardhi kuona kama yanatuma au bado hayajaanza kutumika.
Alisema hilo ni agizo la Rais Magufuli kuona ardhi inatumika kwa tija na kwamba katika maeneo ambayo ukaguzi utabaini mashamba hayo hayatumiki, wizara itatoa taarifa kwa Rais kubadili matumizi ya maeneo hayo na kuwapa wanaohitaji, kwani maeneo mengi yamekaa bila kufanyiwa kazi na wananchi kuyavamia jambo ambalo limeanza migogoro mingi ya ardhi nchini.
Katika ziara yake mkoani Kigoma, Waziri Lukuvi alipokea malalamiko ya ardhi 500 kutoka wananchi wa mkoa huo na katika tathmini yake alisema maofisa ardhi pia wamekuwa wakichangia migogoro mingi ya ardhi inayotokea nchini huku wananchi wakishindwa kutumia njia rasmi za kumiliki ardhi mambo ambayo yamechangia migogoro mingi.
“Nimeshatoa maagizo kwa wasaidizi wangu kuchukua hatua kwa watumishi wa serikali ambao kwa makusudi wamechangia migogoro hiyo ya ardhi, nimeagiza kufanyika pia kwa upangaji, upimaji na utoaji hati ili kuwafanya wananchi kumiliki maeneo salama yasiyo na migogoro,”alisema Waziri Lukuvi.
Katika hatua nyingine Waziri huyo alisema kuwa serikali inafanyia uchunguzi kitendo cha baadhi ya wananchi wachache wa kijiji cha Kagera Nkanda Wilaya ya Kasulu kutengeneza hati feki za ardhi na kujimilikisha hekta 800.
Alisema serikali imebaini hilo baada ya wananchi kulalamikiwa kuingia kwenye maeneo hayo na wamiliki kuonesha kwamba wamiliki hao wanamiliki eneo hilo kihalali wakiwa na hati ambapo baada ya uchunguzi imebainika kuwa hati hizo hazikuwa halali na hivyo kuamuru ardhi hiyo irudi kwa serikali ya kijiji na wananchi waliofanya hivyo wachukuliwe hatua za kisheria za kughushi
Previous
Next Post »