GARI NDOGO YAPIGA MZINGA ENEO LA KIGUZA MKURANGA - Rhevan Media

GARI NDOGO YAPIGA MZINGA ENEO LA KIGUZA MKURANGA


Mwendesha bodaboda akiiangalia Gari ndogo aina ya Toyota Raum yenye namba za usajili T 690 CMS iyopata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kiguza, Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio la ajali hiyo, wanaeleza kuwa Gari hiyo iliyokuwa ikitokea upande wa Hoyoyo kuelekea Mkuranga, iliacha njia na kwenda kugonga mti uliokuwepo kando ya barabara hiyo, kwa madai ya dereva wake kushindwa kuona vizuri baada ya kumulikwa na taa kali ya gari iliyokuwa inakuja mbele yake. Hakuna aliepoteza maisha kwenye ajali hii. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Inavyoonekana gari hiyo baada ya kupiga mzinga.
Break Down au wazee wa kubeba visivyojiweza, wakiipiga cheni gari hiyo.



Previous
Next Post »