Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BENKI ya DCB yaibuka kidedea kwa kupata zawadi ya kwanza kwa sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa hii ni tuzo inayoandaliwa kila mwaka na bvodi ya uhasibu Tanzania (NBAA) ambapo yalianza toka mwaka 2011.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
Mkwawa amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne benki ya DCB imeweza kufanya vizuri kwa kushika nafasi tatu za juu na kuwa moja ya miongoni mwa benki zinazofanya vizuri na katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu na kwa mwaka 2015 imeweza kushika namba moja.
Amesema kuwa benki yao inafuata miongozo ya utawala bora na kuwataka wawekezaji kuwa na imani juu ya usalama wa fedha zao walizoziwekeza na kuahidi kuendeleza mafanikio hayo kiujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akionyesha kifaa kitakachokuwa kinatumiwa na mawakala wa benki hiyo katika mfumo utakaoenda wa DCB PESA unaotarajiwa kuanza Januari 2017.
Mkwawa ameweka wazi mafanikio ya benki hiyoikiwemo ni kutimiza miaka 14 ya utoaji huduma bora za kibenki kwa wajasiliamali, kuongezeka kwa matawi kutoka mawili mwaka 2005 hadi matawi tisa 2016 na mwakani 2017 wanatarajia kufungua tawi la 10 mkoani Dodoma.
Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na mtaji imara wa bilioni 32 na upanuaji na uboreshaji wa huduma za kisasa kwa wateja wetu kupitia mawakal ambapo watawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala walioidhinishwa na DCB katika vitongoji kwa kupitia DCB PESA inayotarajiwa kuanza Januri 2017.
Mawakala wa DCB wakiwa makini kusikiliza.
Sign up here with your email