LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho Ijumaa kwa mchezo Na. 129 utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam utakaochezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na. 1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.
Jumamosi Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ya Mbeya City na Toto African kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.
Mchezo Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.
Ndanda itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo, safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132 utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.
Mchezo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, kati ya
Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga akisaidiwa na Omari Kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.
Sign up here with your email